Friday, August 29, 2008

Kampuni kusuka wanamichezo Olimpiki 2012

KAMPUNI ya Kuhudumia Makontena Bandarini (TICTS), imesema itasimama imara kuhakikisha Tanzania inapata medali katika Michezo ya Olimpiki itakayofanyika London, 2012.
Hayo yalisemwa na Meneja Masoko wa TICTS, Predi Asenga, ambaye alimwakilisha Mkurugenzi wa kampuni hiyo, katika hafla fupi ya kukabidhi bendera na kuwapongeza wanamichezo hao kwa kudumisha nidhamu katika michezo hiyo.

Asenga alisema wanamichezo wa Tanzania walikumbana na ugumu wa michezo kutokana na kukutana na wanamichzo walio na maandalizi ya nguvu, lakini ana imani kwa kadri TICTS watakavyoingia kwenye timu ya 2012, medali zitapatikana.

“Tunataka kufanya maandalizi ya muda mrefu, lazima Tanzania tuibuke na medali michezo ya London, lakini yote ni maandalizi, TICTS tunaliweza hilo na tutahakikisha Tanzania inaweka historia,” alisema.

Wanamichezo wa Tanzania walifanya vibaya katika michezo ya Olimpiki ya Beijing, ambapo kati ya wanamichezo wanane, hakuna hata mmoja aliyeibuka na medali.

''Tuna matumaini, ushirikiano wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), fedha zaidi zinaweza kupatikana kwa ajili ya kuwasaidia wanamichezo wetu, katika michezo ijayo kuelekea michezo ya Olimpiki ya London 2 012. Tutafanya kila tuwezalo kuunga mkono juhudi hizo kwa njia yoyote ile tutakayoweza.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa, BMT, Kanali mstaafu Idd Kipingu, ameipongeza TICTS, hasa kwa kufanimkisha ushiriki wa Tanzania katika michezo hiyo ya Beijing China.
Hafla hiyo iliyoambatana na chakula cha mchana kwa msafara wa wanamichezo wa Olimpiki ukijumuisha waogeleaji pamoja na wanariadha, iliandaliwa na serikali kwa kushirikiana na TICTS, kwenye hoteli ya Travertine, jijini Dar es Salaam.

Kipingu alisema, TICTS ni wapya katika medani ya michezo na kuwa kwa niaba ya serikali, akiwa kama Mwenyekiti wa BMT wanawapongeza na kuwakaribisha katika udhamini wa michezo nchini.

''Hatukupenda mlivyoitwa watalii, tena wengi wao ni Waandishi wa Habari, lakini nasikitika hawakujua nini maana ya Olimpiki, kuna mambo mengi huko ambako walimu, wachezaji wamejifunza…,'' alisema.

Naye Rais wa TOC, Ghulam Rashid, aliahidi kukaa pamoja na kujipanga kwa kuangalia upungufu uliojitokeza katika mashindano ya mwaka huu na kuanza mapema maandalizi ya michezo ijayo ya London 2012.

Pinda aongea

SAUTI za minong'ono zilikuwa zimetanda kwenye Ukumbi wa Bunge jana wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alipokamilisha kusoma hotuba yake ya utekelezaji wa mapendekezo ya Kamati ya Richmond, baada ya hatua kadhaa dhidi ya wahusika kumsubiri rais na watendaji wake.

Uwezekano wa wabunge kujiridhisha kwa kuchangia hotuba hiyo mara baada ya Waziri Mkuu kumaliza kutoa hoja, ulishindikana baada ya Naibu Spika, Anna Makinda, kuzima juhudi hizo akisema wataijadili taarifa hiyo katika kikao kijacho cha Novemba, mwaka huu.

Kati ya mapendekezo hayo ni machache tu ndiyo ambayo utekelezaji wake umekamilika huku mengine muhimu ambayo wabunge na wananchi walikuwa wanayasubiri kwa hamu yakiachwa kwa mamlaka zinazowajibika, likiwamo suala la Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kusubiri hatua atakazochukuliwa na Rais Jakaya Kikwete, huku la Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) likiachwa mikononi mwa Katibu Mkuu Kiongozi.

Nasreen akabidhiwa gari

Nasreen Kharim, mrembo wa taji la Vodacom 2008 muda mfupi baada ya kukabidhiwa zawadi ya gari la kifahari aina ya Grand Vitara yenye thamani ya Sh42 milioni jijini Dar es Salaam Alhamisi.

Monday, August 25, 2008

Yanga wamtundika mtu 4 mnunge


VINARA wa Ligi Kuu msimu uliopita, Yanga na Prisons, wameanza kashkash za Ligi Kuu, huku Yanga ikiwachapa washindi hao wa pili wa Ligi Kuu mabao 4-0 katika mchezo mkali kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Timu nyingine zilizoibuka na ushindi katika mechi zao za ufunguzi wa Ligi Kuu ya Vodacom ni Kagera Sugar iliyoifunga Polisi Moro mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba wakati Moro United iliitandika Azam mabao 3-2 kwenye Uwanja wa Taifa.

Kikwete akiserebuka


Rais Kikwete na mkwewe Mama Salma, wakicheza ngoma kwenye harusi ya mwanao Ridhiwani iliyofanyika Ubungo Plaza.

Saturday, August 23, 2008

Kikwete awaonya TFF

RAIS Jakaya Kikwete amewatahadharisha viongozi wa Shirikisho la Soka (TFF) kuwa hawana budi kuwa makini na fedha wanazopata kwa kuwa kutafuna fedha za chama kunaweza kuifanya serikali kuiingilia kati na hivyo kupoteza uhuru wake wa kujiendesha.

Rais Kikwete pia amewataka viongozi wa TFF kutobweteka msaada wa serikali wa kumlipa kocha wa kigeni na badala yake watafute vyanzo vya fedha kwa ajili ya kugharimia jukumu hilo kwa kuwa si la serikali.

Rais Kikwete, ambaye aliahidi kusaidia kusukuma mbele maendeleo ya michezo nchini, alisema hayo jana wakati akihutubia Bunge la Jamhuri ya Mungano mjini Dodoma jana.
Kikwete alisema TFF isije ikadhani kuwa katika mishahara ya watumishi wa umma, kuna fungu la mshahara wa kocha wa soka.

''TFF wasigeuze ofa yangu kuwa ya milele…suala la kocha si kazi ya serikali. Waanze kujiwekea fungu kwa ajili ya kujijengea uwezo wa kumlipa kocha,'' alisema Kikwete. ''Hizo fedha kidogo wanazopata wasizitafune. Waanze kujiwekea kidogo kidogo; waanze kutengeneza fungu, wasizitafune.

“Pamoja na kwamba kile (TFF) ni chombo cha hiari, wakitafuna fedha watatushawishi tuwaingilie na hivyo watapoteza uhuru wao wa kujiendesha kwa uhuru.”

Kikwete alisema kuwa azma yake na serikali kwa ujumla ni kuona michezo inapiga hatua na hasa soka ndio maana iliamua kutoa msaada wa kiufundi kwa vyama.

Kikwete, ambaye ni shabiki mkubwa wa soka, hakuacha kumwaga sifa kwa timu ya taifa ya soka, Taifa Stars, ambayo alisema sasa imeigeuza nchi kuwa kinyozi baada ya miaka kadhaa ya kuwa kichwa cha mwenda wazimu.

''Nimeleta kocha na nikakubali kumlipa. Hivi sasa Tanzania inafanya vizuri na hivyo si kichwa cha mwendawazimu tena, sasa hivi Tanzania ni kinyozi,'' alisema rais ambaye alikuwa mchezaji wa mpira wa kikapu.

“Nina hakika katika mashindano mengine siku zijazo, kama Cameroon ikipangwa na Tanzania, itaomba ratiba hiyo ibadilishwe. Hata hao Ghana, katika mchezo wa jana (juzi), tumeona mambo yalikuwa magumu kwa Ghana na hadi kipa akaenda kusaidia kufunga.”

TUCTA wasitisha mgomo

SHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), limeahirisha mgomo wake wa siku tatu uliopangwa kuanza kesho kutwa na badala yake litasubiri utekelezwaji wa ahadi ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa juzi bungeni Dodoma.

Kauli hiyo ilitolewa kwa waandishi wa habari Dar es Salaam jana na Katibu Mkuu wa TUCTA, Bw. Nestory Ngulla, baada ya kikao cha makatibu wote wa vyama vya wafanyakazi nchini kutafakari kauli ya Rais Kikwete.

Bw. Ngulla alisema vyama vya wafanyakazi nchini na wafanyakazi wote kwa ujumla, wana imani kubwa na Rais Kikwete, kwa kuwa kauli zake zinaaminika na zina uzito wa pekee kama kiongozi wa Taifa na kuzishutumu kauli alizoziita za kejeli, zilizotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bibi Hawa Ghasia.

"Kauli ya Mheshimiwa Rais hatuwezi kuifananisha na kauli za kejeli na zisizoaminika zilizotolewa na Waziri wa Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bibi Ghasia. "Kauli ya Rais aliyoitoa, lazima ipewe uzito wa pekee, tunaamini ahadi aliyoitoa ya kulipa malimbikizo ya mishahara yanayolalamikiwa na wafanyakazi ya Agosti mwaka huu ni ahadi ya kweli," alisema.

Katibu Mkuu huyo, alisema baada ya kuona uzito wa ahadi aliyotoa Rais Kikwete, kikao cha TUCTA kilichokutana jana kilipitisha uamuzi wa dhati wa kuahirisha mgomo huo uliopangwa kufanyika siku tatu mfululizo kuanzia Agosti 25 hadi 27 mwaka huu, hadi hapo ahadi ya Rais itakaposhindikana kutekelezwa kwa muda alioeleza.

Alisema notisi ya mgomo iliyotolewa awali inaendelea kufanya kazi na itasubiri hadi Septemba 3 mwaka huu, siku ambayo Rais ameahidi kumaliza tatizo hilo na kama hakuna utekelezaji, mgomo utaanza mara moja.

Ridhiwani apata jiko

Rais Kikwete akiwapongeza maharusi muda mfupi baada ya kufunga ndoa, ubungo plaza.
Mama Kikwete apimpa mkono wa pongezi mkwe wake, Arafa.

Mwanasheria Ridhiwani Kikwete akiwa na mkewe Arafa mudas mfupi baada ya kufungua pingu za maisha jana usiku Ubungo Plaza.



Thursday, August 21, 2008

Wabunge wataka muungano ufutwe

MJADALA wa Muungano umeingia katika sura mpya baada ya wabunge kuibua madai ya kutaka iundwe serikali moja ya Muungano badala ya mfumo wa sasa wa serikali mbili.
Kauli hiyo ya wabunge imetolewa wakati tayari Muungano umekuwa ukitikiswa kwa nguvu kutokana na hoja ya Zanzibar si nchi au la.

Wakichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), kwa nyakati tofauti wabunge hao, wengi wao wakiwa wanatoka Bara walisema, dawa pekee ya Muungano huo ni kuundwa kwa serikali moja ya Jamhuri ya Muungano, ingawa dawa hiyo ni chungu.

“Dawa pekee ya Muungano ni kuelekea katika serikali moja ya Jamhuri ya Muungano, ingawa dawa hiyo ni chungu lakini hii ndio italeta Utanzania wa kweli, badala ya kuwa na serikali mbili au tatu,” alisema Mbunge wa Mchinga (CCM), Mudhihir Mudhihir.

Mudhihir alisema, mtafaruku unaoendelea sasa kutokea bungeni, ni mazoea na tamaa za utawala kwa baadhi ya viongozi na kulazimisha kulumbana kwa kugombea majina au serikali kila upande, jambo ambalo halina mantiki kwa sababu majina hayo (Tanganyika na Zanzibar) hakuna anayejua maana yake.

Bolt avunja record ya dunia


Usain Bolt, raia wa Jamaica, awa bingwa mpya wa mbio fupi za mita 100 duniani baada ya kutumia sekunde 19.30 na kuvunja ile iliyo wekwa na bingwa wa zamani Michael Johnson aliyetumia sekunde 19.32, Bolt ameshinda Medali ya dhahabu

Bolt akiwa aamini macho yake baada ya kuibuka mshindi

Bolt akiwa na Bendera ya nchi yake ya Jamaica akisalimiana wa wapenzi wake baada ya kushinda mbio fupi za mita 100


Usain Bolt akiwa amepoz katika picha huku bango likiwa linaonyesha rekodi mpya ya dunia iliyowekwa naye ye mwenyewe.





Tuesday, August 19, 2008

Wakatoliki wazuiwa kumpokea Milingo


RAIS wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC) Mhashamu, Askofu Thadeus Rwaichi amewataka waumini wa kanisa hilo kutoshiriki katika ujio wa aliyekuwa Askofu wa Jimbo la Lusaka, Zambia Emmanuel Milingo anayetarajiwa kuzuru nchini hivi karibuni.


Askofu Rwaichi alitoa tahadhari hiyo juzi mjini hapa wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya ujio wa Askofu Milingo anayetarajiwa kuzuru nchini kati ya Agosti 22 na 25 mwaka huu.


Alisema hatua hiyo inatokana na matukio kadhaa yaliyofanywa na askofu huyo kwenda kinyume na maadili ya kanisa hilo kwa kuamua kuoa .


Askofu Rwaichi, alisema kutokana na kitendo hicho, waumini wa Kanisa Katoliki hawana sababu ya kushiriki katika ujio huo kwani hauna uhusiano wowote na kanisa hilo .


Aidha, alisema hata kama wapo waumini ambao watashiriki kwenye ujio huo watambue wazi kuwa kufanya hivyo ni kinyume na maamuzi ya kanisa hilo. "Naomba kusema kuwa waumini wangu msikengeuke, hata kama wapo watakaoshiriki ujio wa Askofu Milingo lazima wajue wanasimama wapi kwa kuchukua tahadhari kubwa,”alisema Askofu Rwaichi.


Alibainisha kuwa kwa sasa kuna tetesi kwamba Askofu Milingo anaishi nchini Korea baada ya kuasi Kanisa lake kwa kuamua kuoa jambo ambalo ni kinyume na kanisa hilo .

Kikwete apokea riport ya EPA "kisailensa"


RIPOTI ya uchunguzi wa tuhuma za ufisadi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imekamilika, kwa kukabidhiwa kimyakimya kwa Rais Jakaya Kikwete.


Kukabidhiwa kimyakimya kwa ripoti hiyo jana bila kuwepo waandishi wa habari, kunazidi kuweka wingu na kuibua maswali mengi kuhusu mchakato mzima wa uchunguzi huo.


Matokeo ya EPA yamekuwa yakisubiriwa kwa hamu na nchi 11 wafadhili zinazochangia katika Mfuko Mkuu wa Bajeti (GBS), ambazo zimesitisha utoaji wa sehemu ya fedha zake zikitaka hatua zaidi zichukuliwe kwa watuhumiwa kutoka makampuni 22 yaliyoiba kiasi hicho cha zaidi ya Sh 133 bilioni.


Wafadhili, sawa na wananchi walio wengi wanataka kuona hatua zaidi zinachukuliwa kwa wahusika wote wa ufisadi katika EPA.


Kubwa ambalo hadi sasa linasubiriwa, ni kuona na kusikia majina ya wahusika wa ufisadi huo wa mabilioni ambayo yameibwa katika taasisi nyeti ya fedha ya nchi.


Hata hivyo, wakati matumaini yakiwa ni hayo siku ya jana ambayo ilikuwa ni muhimu kwa waandishi kuweza kuhoji na kupata ufafanuzi wa baadhi ya mambo kuhusu mchakato mzima wa uchunguzi huo wa EPA, kiu hiyo haikukidhiwa baada ya timu kukabidhi ripoti kimyakimya.


Kwa mantiki hiyo, kitendo cha waandishi kutokuwepo katika tukio hilo la Rais kukabidhiwa ripoti kuliwanyima fursa wananchi kupata taarifa sahihi ambazo zingetokana na maswali ya waandishi kwa wajumbe wa timu na hata Rais.

KP leo


Monday, August 18, 2008

Mkapa akemea Majungu


"Hawayaoni mema ya wenzao bali kutangaza mabaya, nakerwa na maneno ya vijiweni, yatagawa Watanzania, cha msingi ni kuibua vipaji vitakavyolinda amani ya nchi" hayo ni maneno ya rais mstaafu wa awamu ya tatu Mh. Benjamini Mkapa aliyoisema jana akizungumza kwenye Jubilei ya Kuadhimisha Miaka 100 ya Ukristo Jimbo Katoliki la Singida iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu..
Alisema Watanzania wana imani, dini na makabila mbalimbali, lakini ni vyema kila mtu akatumia kitu hicho kudumusha amani na utulivu.
"Kuna watu hawataki kuona mema ambayo yamefanywa na mtu badala yake wako tayari kutangaza mabaya tu aliyofanya ili kuvuruga umoja na amani," alisema Rais huyo mstaafu na kuongeza "Mambo mema yanatuunganisha lakini si mabaya."
Bw. Mkapa ambaye mara nyingi alikuwa akitumia maneno ya dini na kunukuu vifungu vya Bibilia, alisema "Inapendeza ndugu wakipendana na kukaa pamoja kwa lengo la kupanua wigo na kuongeza imani ya Ukristo."
Awali Askofu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu Dar es Salaam Muadhama Polycarp Kadinali Pengo aliwataka Watanzania kupeleka ujumbe wa amani kwa wanaotumia silaha kwa lengo la kuvuruga amani.
Kadinali Pengo, alisema Bara la Afrika limegubikwa na mambo mengi mabaya hivyo kanisa haliwezi kukaa kimya bali litahakikisha linapeleka ujumbe wa amani, upendo kazi ambayo ilianzishwa na wamisionari kutoka Ulaya

Rushaka basi Olimpiki

MUOGELEAJI wa Tanzania, Khalid Yahya Rushaka jana alishika nafasi ya tatu kwenye michuano ya awali ya kuogelea lakini akashindwa kusonga mbele baada ya kumaliza mchezo wa mita 50 akiwa nje ya muda unaotakiwa.

Rushaka, ambaye alishiriki mchezo wa kuogelea wa mita 50 (freestyle) alitumia muda wa sekunde 28.50 ambao ni tofauti ya sekunde 7.04 wa muda wa kufuzu kwenda raundi ya pili na hivyo kutupwa nje ya mashindano hayo.

Kwa mujibu wa tovuti ya Olimpiki, Rushaka alishiriki mchuano wa mchujo akiwa Kundi la tatu na akashika nafasi ya tatu akiwa nyuma ya muogeleaji wa Malawi, Charlton Nyirenda, aliyetumia sekunde 27.46 na Jackson Niyomugabo wa Rwanda aliyetumia sekunde 27.74.

Kundi hilo halikuweza kutoa muogeleaji wa kwenda raundi ya pili baada ya wote kuwa chini ya muda wa kufuzu.


Thursday, August 14, 2008

Maisha yasiyo bora



Mkazi wa Kurasini Zam Cargo, Joyce Mathias, akiwa amekaa katika eneo la wazi na familia yake wakati nyumba zikiendelea kuvunjwa kupisha upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam jumatano.Wakazi hao waliilalamikia Bandari kwa madai ya kutowalipa sehemu ya fedha wanazoda.

Wednesday, August 13, 2008

Naomba Mkono Afande

TUSAIDIENI AFANDE! Mwanafunzi John Makonyora wa shule ya Sekondari Kambangwa, akizungumza na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu, Dar es Salaam, Bw. Suleiman Kova, alipofanya ziara ya ghafla katika Kituo cha Daladala cha Mwenge kupata taarifa mbalimbali kutoka kwa wananchi zitakazosaidia kuondokana na kero za usafiri.

Tuesday, August 12, 2008

KP leo


Nini kimemsibu Angela Lubala

Balozi wa Redd's 2008 Angela Lubala, amelirudisha taja lake alilokuwa amelishinda katika kinyang'anyiro cha Vodacom Miss Tanzania 2008.

Angela alisema amefikia uamuzi huo kutokakana na imani yake ya dini ya World Alive International Outreach lililopo Sinza, jijni Dar.

“Nachukua fursa hii kuiambia jamii kuwa kutokana na imani yangu katika Yesu Kristo, sitaweza kuwakilisha Redd’s kama Redd’s Fashion Ambassador 2008, Kwa kuwa mimi si mbinafsi, narudisha taji hili na zawadi zake zote kwa Redd’s, napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Vodacom, Lino na Redd’s kwa uelewa juu ya uamuzi wangu huu”, alisema.

Vodacom ndio wadhamini wakuu wa Miss Tanzania. Angela ambaye pia ni Miss Temeke 2008, alisema zawadi anayorudisha ni fedha sh. Milioni 2.5.

Alipoulizwa kama hakujua wakati anashiriki mashindano hayo tangu mwanzo kama kuna jambo kama hilo, alisisitiza kuwa suala la kuwa Balozi wa kinywaji hicho haliendani na imani yake.

Mgosi ndani ya Taifa Stars

KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, Mbrazil Marcio Maximo, jana alitangaza kikosi cha wachezaji 28 huku akiwarejesha kundini Mussa Hassan Mgosi na kumwita kwa mara ya kwanza kipa Amani Simba.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Maximo alisema uteuzi wake umezingatia kiwango cha mchezaji, umri na nidhamu ya nje na ndani ya uwanja.

Alisema kwa kigezo cha umri, ni katika mkakati wa kuunda kikosi kitakachodumu kwa muda mrefu, hivyo asilimia 60 ya wachezaji ni wa chini ya miaka 23, asilimia 20 wa chini ya miaka 20 huku asilimia 20 wakiwa ni zaidi ya miaka 25.

Nyota waliomo katika kikosi hicho na timu zao katika mabano, ni makipa Ivo Mapunda (Yanga), Amani Simba (Simba) na Farouk Ramadhani (Miembeni).


Mbeki ni Shadrack Nsajigwa, Fred Mbuna, Amir Maftah na Nadir Haroub ‘Cannavaro’ (Yanga), Juma Jabu, Kelvin Yondani na Meshack Abell (Simba) na Salum Sued (Mtibwa).


Viungo ni Henry Joseph Shindika, Jabir Aziz na Adam Kingwande (Simba), Godfrey Boniface na Athumani Idd ‘Chuji’ na Kiggi Makasi (Yanga), Nizar Khalfani (Moro United), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar).


Washambuliaji ni Mgosi (Simba), Uhuru Selemani (Mtibwa Sugar), Jerrison Tegete na Mrisho Ngassa (Yanga). Aidha, Maximo amewaita chipukizi watano kutoka mashindano ya Copa Coca Cola na kikosi cha chini ya miaka 20, ambao ni Jonas Salvatory, Yousuf Soka, Adili Adam, Lambele Jerome na Awasi Issa.

Baba Mtakatifu ataka kuondolewa kwa majeshi Georgia


Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Baba Mtakatifu wa kumi na sita, ameonya kuwepo ongezeko la wakimbizi na hata watu kuyakosa makazi yao huko Georgia, kutokana na majeshi yaliyo ingia nchini humo kutoka Urusi.


Kutokana na hilo basi, Baba Mtakatifu huyo ameomba kuondolewa kwa majeshi ya kivita nchini humo ili kurudisha amani ambayo inatoweka, na kuwakutanisha viongozi wa Urusi na Georgia, "Ni matumaini yangu makubwa kuwa shughuli hizi za kivita nchini Georgia zitasimamishwa haraka" alisema.


"Ninaialika jumuiya ya kimataifa kwa ujumla na nchi mbalimbali, kusaidia kupatikana kwa suluhisho juu ya tofauti kwa nchi hizi mbili na kuleta amani ya kudumu na kufikia muafaka kati ya pande zote mbili ambao utakuwa wa sawa na haki na wa heshima.




TUCTA kulitikisa Taifa

Shirikisho la vyama vya wafanyakazi (TUCTA), limesema serikali imepoteza mwelekeo, hali ambayo imewalazimisha waandae mgomo wa siku tatu utakaolitikisa taifa siku 13 zijazo.

Tamko hilo la TUCTA lilitangazwa jana jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa shirikisho hilo, Nestory Ngulla, wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Hatua hiyo ya TUCTA ilitangazwa jana wakati serikali ikifanikiwa kuzima mgomo mwingine wa madaktari wanafunzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ulioanza mwishoni mwa wiki na ambao jana ulikuwa ukitarajiwa kuwaunganisha wauguzi.

Ngula aliongeza kuwa iwapo serikali haitasikiliza kilio cha wafanyakazi hao na baada ya siku hizo tatu, wataandaa mgomo mwingine ambao utakuwa mkubwa zaidi na wenye madhara zaidi kwa uchumi wa Tanzania.

“Mgomo wetu ni wa siku tatu na kama hatutasikilizwa, tutaufanya mwingine mkubwa zaidi ambao tuna hakika utalitikisa taifa hili changa lenye viongozi wasiojali masilahi ya wafanyakazi,” alisema Ngulla.

Alisema malimbikizo ambayo mpaka sasa wanadai ni sh bilioni 500, ambazo kila siku wamekuwa wakipewa ahadi ya kulipwa na serikali lakini hawalipwi, na mambo yanakwenda kisiasa zaidi.

“Wafanyakazi ni wavumilivu sana lakini kwa hivi sasa uvumilivu wetu umefikia kikomo, kwani tunatumia nguvu nyingi lakini hakuna tunachokiambulia,” alisema Ngulla.

TTCL yageuzwa ‘shamba la bibi’


HADI mwaka 2010, kampuni ya kigeni ya Saskatel inayosimamia uendeshaji wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) itakuwa imejichotea Sh. 38 bilioni, imefahamika.


Saskatel ni kampuni ya Canada iliyoingia mkataba wa miaka mitatu na serikali ya Tanzania katikati ya mwaka jana, ikiwa ni miaka miwili baada ya TTCL kuzamishwa kutokana na mkataba wa kwanza uliowaingiza MSI/Detecon na kutekelezwa “kishkaji.”


Taarifa za ndani ya TTCL na serikalini zimesema mkataba mpya una matatizo mengi yanayozidisha utafunaji wa fedha za kampuni hiyo iliyokuwa na mtandao madhubuti wa simu za mezani ambao ulienea nchi nzima.


TTCL iliyokuwa na mali zisizohamishika za thamani ya zaidi ya Sh. 500 bilioni, sasa imebaki kama mjane aliyenyang’anywa mali ya urithi.


Majengo, mitambo na viwanja ambavyo vilikuwa mali ya TTCL vilinyofolewa kwenye kampuni. Hazina kubwa ya wataalamu katika kada mbalimbali za ufundi katika Chuo cha Posta cha Kijitonyama, Dar es Salaam nayo ilibomolewa, chuo kusambaratika na mitambo yake kung’olewa.


Vyanzo vya habari vimebainisha kuwa moja ya matatizo katika mkataba wa Saskatel na serikali ni kuhusu gharama za kutunza maofisa wa Saskatel na familia zao.


Jumla ya maofisa 12 wazungu ambao waliletwa nchini kwa madai kuwa ni wataalam wa Saskatel, wanalipwa na kuhudumiwa na TTCL kwa muda wote wa mkataba badala ya kugharimiwa na Saskatel.


“Saskatel wana mkataba. Kama wanaleta wataalam, basi ni wao wanaostahili kuwalipa na siyo TTCL. Gharama za kuwaleta nchini, kuwatunza wao na familia zao na hata gharama za likizo zao, vyote vinategemea TTCL. Kwa nini?” Anauliza ofisa mmoja mwandamizi wa shirika hilo.


Kadhalika, wakuu wa idara na vitengo ambao ni Watanzania, walioajiriwa kwa mkataba na Saskatel, nao wanalipwa mishahara kwa fedha zinazozalishwa na TTCL.


Hata pale kazi za Saskatel zinapokwama kwa sababu ya majanga ya kimaumbile – kwa mfano mafuriko na tetemeko la ardhi yatakayosababisha kuharibu mtandao wa mawasiliano – gharama za kurudisha mtandao, zinapaswa kulipwa na TTCL, unaeleza mkataba.


Tatizo jingine ni kipengele kinachotaka Saskatel walipwe kila baada ya mwaka mmoja “malipo ya ada ya mafanikio” lakini haielezwi ni vigezo gani vitatumika kupima mafanikio hayo na utaratibu upi wa kupanga malipo yake.


Kwa hali yoyote ile, hii ni njia ya kuchuma kwenye “shamba la bibi” kama walivyofanya MSI/Detecon na kujenga himaya ya Celtel ya kimataifa.


Kampuni ya Celtel ilichipuka katika MSI/Detecon; ikitumia mitambo ya mawasiliano ya TTCL na kujitanua hadi nchi za Uganda na Kenya kabla ya kusambaa nchi nyingine jirani.


Kwa kutumia kiini kilekile cha Tanzania, Celtel ilijibadilisha na kuwa Celtel International na baadaye kujitanua na kuwa mwanachama wa kundi la makampuni ya MTC (Mobile Telecommunication Company) ya Ghuba.


Hivi karibuni, Celtel International imejibadilisha na kuwa ZAIN. Yawezekana Saskatel inajiwekea msingi kutoka shamba lilelile la “bibi” ambako mikataba imekuwa haizingatii maslahi ya raslimali za Watanzania.


“Sikiliza ndugu yangu; wanaoingia mikataba hii wanajua wanachofanya. Wanawekeza hukohuko. Hatuwezi kulaumu watu wa nje peke yao maana hii hujuma inaanzia hapa kwetu,” ameeleza ofisa huyo.


Kwa mujibu wa taarifa zilizoifikia MwanaHALISI, tayari Saskatel imepeleka ripoti kwao kuelezea “utekelezaji wa mkataba,” kitendo kinachoashiria kuanza hatua za kudai na kuchota malipo ya kwanza.


Kwa mujibu wa mkataba, Serikali ya Canada ndio mdhamini wa mkataba kwa Saskatel, na utaratibu unaelekeza serikali ndizo zitawajibika kuwasiliana kuhusu malipo hayo.


Lakini kumezuka utata hapo, kwa kuwa waliyoyaeleza hayakuidhinishwa na Bodi ya Wakurugenzi ya TTCL inayoongozwa na Profesa Mathew Luhanga.


Kwa sababu hiyo, inasemekana Profesa Luhanga amelalamika na kuna mvutano kati ya Bodi na wakuu wa Saskatel.


Taarifa zaidi zimesema Saskatel wamejipendelea kwa kuwa hata kwa yale maeneo yasiyoleta tija yoyote kwa TTCL, wametaja kama yamefanikiwa.


Wakati miradi karibu yote ya maendeleo iliyopangwa na TTCL katika mpango wake wa maendeleo tangu mwaka 2006 imekwama baada ya kupuuzwa na wawekezaji, Saskatel wamesema wameitekeleza vema.


Baadhi ya maeneo wanayodai yamepiga hatua kutokana na utaalamu waliotoa, ni kuongeza laini 7,347 za simu za kulipia kabla na laini 7,122 za kulipia baada ya kutumia.


Ripoti ya Saskatel imebainisha mafanikio katika mtambo wa kuandaa bili za wateja (CCBS) wakati mtambo huo haufanyi kazi.


Mafanikio mengine yanayotajwa ni ufanisi katika kutengeneza simu ndani ya saa 24 baada ya wateja kuripoti hitilafu.Eneo jingine ambako Saskatel haikusema ukweli, ni kuhusu maslahi ya wafanyakazi wa TTCL. Hadi sasa hakuna maafikiano kati ya menejimenti na wafanyakazi juu ya muundo wa mishahara.


Kinachoonekana ni juhudi za menejimenti kuwagawa wafanyakazi kwa misingi ya mishahara na marupurupu; hatua ambayo imesababisha wasiwe na umoja katika kudai haki zao.


Kwa mfano, viwango vya mishahara vilivyowekwa, vinatofautiana sana kutoka tabaka la juu la mameneja hadi la chini.


Saskatel waliingia TTCL baada ya kujengewa mazingira na wawekezaji wa awali – MSI/Detecon – ambao wakati wanaondoka, walipendekeza TTCL iendeshwe na kampuni inayojitegemea. Saskatel ilikuwa kampuni ya ununuzi wa zana zilizotumiwa na MSI/Detecon.


Kulingana na vyanzo mbalimbali vya taarifa, wakati Saskatel wanaingia TTCL, hesabu zilizoishia 31 Desemba 2006 zilikuwa zinaonyesha kampuni iliingiza mapato ya Sh. 92.018 bilioni na mapato kabla ya kodi na riba yalikuwa Sh. 16.210 bilioni.


Kwa mujibu wa waraka uliosomwa kwa Kamati ya Bunge ya Miundombinu mwaka jana, TTCL ilikusudia kuimarisha huduma za simu na kupanua mtandao wa mawasiliano nchi nzima kwa kutumia bajeti ya Sh. 212 bilioni.


Miongoni mwa miradi hiyo ni kusambaza simu za mkononi zisizotumia waya (CDMA). Simu hizo zilizotakiwa kuenea kwenye miji mikuu ya mikoa na wilaya kote Bara na Zanzibar ifikapo Juni 2007.


Kuingia kwa Saskatel hakujaleta nafuu. Mradi huo haujatekelezwa hata ndani ya Dar es Salaam kwenyewe ambako mtandao wake ni duni mno.


MwanaHALISI lina taarifa kuwa mali za TTCL zisizohamishika zimefisidiwa kiasi kwamba baadhi ya nyumba zake ziliuzwa kwa bei ya kutupa kupitia iliyokuwa kampuni ya Simu 2000 Ltd.


Kwa mfano, imeelezwa kuwa nyumba aliyokuwa akitumia Mkurugenzi Mkuu wa TTCL iliyoko mtaa wa Chake Chake eneo la Masaki Dar es Salaam, iliuzwa kwa kiasi cha Sh. 20 milioni wakati thamani yake ilikaribia Sh. 500 milioni.


Nyumba hiyo, kwenye kiwanja Na. 308 aliuziwa Marten Lumbanga, Balozi wa Tanzania nchini Uswisi ambaye wakati wa mchakato wa kubinafsisha TTCL ikiwemo uuzaji wa mali zake kupitia Simu 2000 Ltd, alikuwa Katibu Mkuu Kiongozi.


Nyumba nyingine za TTCL zilizouzwa kwa “bei poa” zipo Kurasini, Chang’ombe, Upanga, Ilala na Oyster Bay. Nyingine zipo kwenye makao makuu ya wilaya nchini kote ambako pia kuna viwanja vyake.


Wiki iliyopita, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Dk. Maua Daftari aliliambia Bunge kuwa serikali imepata Sh. 18.327 bilioni kutokana na uuzaji mali za TTCL uliofanywa na iliyokuwa kampuni ya Simu 2000 Ltd.


Waziri hakusema ni mali zipi ziliuzwa, ingawa mali zilizothibitishwa kuwa ni za TTCL alisema ni majengo 103 na viwanja 30.


Alikuwa akijibu swali la Victor Mwambalaswa (Lupa, CCM) aliyetaka kujua mali za TTCL zilizohodhiwa na Simu 2000 Ltd na kiasi gani kilipatikana baada ya kuuzwa.

Shaggy Kipenzi cha wa Tz


LICHA ya kukonga nyoyo za mashabiki msanii Norville Rogers au Shaggy mwisho wa wiki kwenye viwanja vya Leaders, Dar es Salaam alitumia muda huo kukemea vitendo vya ubaguzi wa rangi na kijinsia na kusisitiza upendo.
Msanii huyo aliyezaliwa Jamaica na kuhamia Marekani anakoishi sasa, alikuwa akitumbuiza katika onyesho la uzinduzi wa kampuni mpya ya simu za mikononi ya Zain ambayo awali ilikuwa ikitumia jina la Celtel.
Shaggy ambaye ana albamu kumi hadi sasa, alikonga nyoyo za mashabiki na kila baada ya nyimbo mbili au tatu alikuwa akitoa somo.
"Tusibaguane jamani sisi sote ni binadamu, tusibaguane kutokana na rangi, jinsia au hali yetu ya kimaisha,"alisema msanii huyo ambaye alitumbuiza kwa zaidi ya saa mbili kutokana na shinikizo la mashabiki.

Monday, August 11, 2008

Wadau wa Gatundu



Wadau, Idd Shirima na kakili wakiwa katika kuperuzi blog yetu watanganyika, huku wakitumia internet yenye kasi iliyounganishwa na mtandao wa Vodacom 3G.

Tibaigana Anyang'anywa gari na serikali

Serikali imelichukua gari alilolimilki likiwa na utata, Kamanda wa zamani wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Alfred Tibaigana.

SAKATA la mauaji yenye utata ya vijana wawili, wakazi wa Dar es Salaam, Mine Chomba na Hija Shaha Salehe, yaliyotokea mwaka 2006, limechukua sura mpya baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrance Masha, kuagiza magari yote yaliyohusishwa na mauaji hayo, likiwamo analomiliki Kamanda wa zamani wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Alfred Tibaigana, kurudishwa ili uchunguzi ufanyike upya.

Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Waziri Masha, zinaeleza kuwa, magari hayo tayari yamesharejeshwa kwa ajili ya kufanyika uchunguzi kuhusiana na jinsi yalivyochukuliwa.
Inaelezwa kwamba, magari hayo yanayodaiwa kuwa mali ya marehemu Chomba, yalikamatwa na Polisi kwa muda mrefu, yakidaiwa kuwa ni ya wizi kabla ya kuuzwa kwa njia ya utata.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu juzi, Waziri Masha alisema kuwa, magari hayo yote yamesharudishwa kama alivyoagiza.

"Kama mlisikia wakati wa hotuba ya bajeti yangu bungeni, niliagiza magari yote yarudishwe na tayari yamesharudishwa," alisema Waziri Masha.
Kati ya magari hayo yaliyopaswa kurudishwa ni pamoja na Toyota RAV 4 ambalo lilinunuliwa kwenye mnada wa hadhara na Tibaigana.

Hata hivyo, habari zilizopatikana kutoka kwa ndugu wa marehemu Mine, zinaeleza kuwa, tayari walishakwenda kumwona Waziri Masha kujua hatima ya suala la ndugu yao.

Mmoja wa ndugu hao, ambaye hakupenda kutajwa jina lake, alisema kuwa, walikwenda hivi karibuni kumwoma Waziri Masha na kwamba alisema ameshalishughulikia suala hilo kwa kuagiza magari hayo yarejeshwe.

KP leo


Dr. Rashid ahusishwa na kashfa za Rada


Aliyewahi kuwa Gavana wa benki kubwa Tanzania na mkurugenzi wa Vodacom ambaye sasa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Dr. Idris Rashid, amehusishwa na kashfa ya ununuzi wa rada inayochunguzwa na makachero wa Uingereza.


Kwa mujibu wa taarifa za Shirika la Uchunguzi wa Makosa ya Jinai – Serious Fraud Office (SFO) la Uingereza, Dk. Rashid ni mmoja wa watuhumiwa wa ufisadi katika ununuzi wa rada iliyogharimu kiasi cha Sh. 40 bilioni.


Shirika hilo linadai kuwa bei ya rada ilikuwa kubwa kuliko thamani yake na kwamba BAE itakuwa ililipa mawakala kiasi kikubwa cha fedha “kulainisha” baadhi ya viongozi wa serikali ili wakubali bei hiyo.


Dk. Rashid aliteuliwa na Rais Kikwete Novemba 2006 kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO. Mwaka mmoja baadaye, Dk. Rashid aliandika barua ya kujiuzulu lakini rais alimkatalia kujiuzulu.


Uamuzi wa Dk. Rashid kujiuzulu ulitokana na kile alichoita kuamrishwa na Edward Lowassa, aliyekuwa waziri mkuu, kurudisha umeme aliokuwa ameamua ukatwe, katika kiwanda cha Tanga Cement, jambo ambalo Dk. Rashid alilichukulia kuwa “uingiliaji katika kazi na udhalilishaji.”


Taarifa za kuaminika zinasema Dk. Rashid anamiliki kampuni yenye akaunti nchini Uingereza na kwamba kampuni yake ilimegewa Paundi 600,000 za Uingereza (sawa na Sh. 1.32 bilioni) kutoka akaunti ya kampuni ya Andrew Chenge ambaye tayari anachunguzwa na SFO.


Taarifa za kampuni ya Siemens Plessey System (SPS) zinasema, Dk. Rashid anatajwa kuwa mratibu mkuu wa “taarifa zote kutoka serikalini na BoT.” SPS ndio walihusika kufanya majadiliano ya awali ya ununuzi wa rada hiyo kwa niaba ya Serikali, chini ya ofisa wake aliyetajwa kuwa ni Jonathan Joseph Horne.


Wachina sasa wamezidi

Kwa wale walio bahatika kama kuangalia ule ufunguzi wa mashindano ya Olympics live nadhani mlijionea wenyewe jinsi fataki zilivyokuwa zinarushwa hapa na pale.

imethibitika kuwa zile hazikuwa fataki halisi bali zilikuwa ni geresha tu za watu wanaojua kutumia kinakilishi (Computer).

Walifanya ivyo ili kunusuru maisha ya wale waliokuwa wakishuti yale matangazo ya moja kwa moja kwakutumia Chopper yaani ndenge ya mapanga (helicopter).

Nadhani tukipewa chansi ya "ku-hosti" ivi vitu inabidi tuyaangalie haya vizuri.

Sunday, August 10, 2008

Mnauye aweza ukosa Uenyekiti UVCCM


Nape Mnauye yuko kwenye wakati mgumu katika kinyang'anyiro cha Uchaguzi mkuu wa uenyekiti Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), baada ya hoja ya umri kuibuliwa.

Nape alisema haogopi mchezo mchafu wa wapinzani wake kwa kuwa alipoamua kuchukua fomu alikuwa na akili timamu na akizifahamu kanuni, sheria na katiba ya umoja huo vyema, alisema hayo katika mahojiano na chombo kimoja cha habari.

“Kati ya wagombea wote zaidi ya 20 mimi ndiye mwenye uzoefu mkubwa katika chama na jumuiya ya vijana, nimekuwa mjumbe wa NEC kwa muda wa miaka sita, Mjumbe wa baraza la kuu la UVCCM kwa miaka sita na Katibu Msaidizi Idara ya Siasa Makao Makuu ya Chama, najua kanuni, sheria na katiba ya chama ya umoja wa vijana” alisema.

Bernie Mac afariki dunia



Muigizaji wa sinema kutoka marekani, afariki dunia Jumamosi asubuhi akiwa na miaka 50. Mac aliwahi kushiriki muvi mbali mbali zikiwemo za comedy pamoja na vita.