Monday, August 18, 2008

Mkapa akemea Majungu


"Hawayaoni mema ya wenzao bali kutangaza mabaya, nakerwa na maneno ya vijiweni, yatagawa Watanzania, cha msingi ni kuibua vipaji vitakavyolinda amani ya nchi" hayo ni maneno ya rais mstaafu wa awamu ya tatu Mh. Benjamini Mkapa aliyoisema jana akizungumza kwenye Jubilei ya Kuadhimisha Miaka 100 ya Ukristo Jimbo Katoliki la Singida iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu..
Alisema Watanzania wana imani, dini na makabila mbalimbali, lakini ni vyema kila mtu akatumia kitu hicho kudumusha amani na utulivu.
"Kuna watu hawataki kuona mema ambayo yamefanywa na mtu badala yake wako tayari kutangaza mabaya tu aliyofanya ili kuvuruga umoja na amani," alisema Rais huyo mstaafu na kuongeza "Mambo mema yanatuunganisha lakini si mabaya."
Bw. Mkapa ambaye mara nyingi alikuwa akitumia maneno ya dini na kunukuu vifungu vya Bibilia, alisema "Inapendeza ndugu wakipendana na kukaa pamoja kwa lengo la kupanua wigo na kuongeza imani ya Ukristo."
Awali Askofu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu Dar es Salaam Muadhama Polycarp Kadinali Pengo aliwataka Watanzania kupeleka ujumbe wa amani kwa wanaotumia silaha kwa lengo la kuvuruga amani.
Kadinali Pengo, alisema Bara la Afrika limegubikwa na mambo mengi mabaya hivyo kanisa haliwezi kukaa kimya bali litahakikisha linapeleka ujumbe wa amani, upendo kazi ambayo ilianzishwa na wamisionari kutoka Ulaya

No comments: