Tuesday, August 12, 2008

TUCTA kulitikisa Taifa

Shirikisho la vyama vya wafanyakazi (TUCTA), limesema serikali imepoteza mwelekeo, hali ambayo imewalazimisha waandae mgomo wa siku tatu utakaolitikisa taifa siku 13 zijazo.

Tamko hilo la TUCTA lilitangazwa jana jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa shirikisho hilo, Nestory Ngulla, wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Hatua hiyo ya TUCTA ilitangazwa jana wakati serikali ikifanikiwa kuzima mgomo mwingine wa madaktari wanafunzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ulioanza mwishoni mwa wiki na ambao jana ulikuwa ukitarajiwa kuwaunganisha wauguzi.

Ngula aliongeza kuwa iwapo serikali haitasikiliza kilio cha wafanyakazi hao na baada ya siku hizo tatu, wataandaa mgomo mwingine ambao utakuwa mkubwa zaidi na wenye madhara zaidi kwa uchumi wa Tanzania.

“Mgomo wetu ni wa siku tatu na kama hatutasikilizwa, tutaufanya mwingine mkubwa zaidi ambao tuna hakika utalitikisa taifa hili changa lenye viongozi wasiojali masilahi ya wafanyakazi,” alisema Ngulla.

Alisema malimbikizo ambayo mpaka sasa wanadai ni sh bilioni 500, ambazo kila siku wamekuwa wakipewa ahadi ya kulipwa na serikali lakini hawalipwi, na mambo yanakwenda kisiasa zaidi.

“Wafanyakazi ni wavumilivu sana lakini kwa hivi sasa uvumilivu wetu umefikia kikomo, kwani tunatumia nguvu nyingi lakini hakuna tunachokiambulia,” alisema Ngulla.

1 comment:

Anonymous said...

ebwana gomeni hao watu wa serikali yetu ya kibongo wamezidi kula wenyewe kila siku tuna sikia mbunge fulani fisadi,mnapeana wenyewe kwa wenyewe halafu likigundulika mnajifanya kujiuzulu sasa zamu ya kujiuzulu wafanya kazi sasa halafu tuone itakuwaje tena mm naona kama hizo siku tatu ndogo sana hasira zitakuwa hazijaisha mngeongeza nne mkamilishe wiki au mnaonaje wazee wasipo lipa mnaongeza mwezi mzima hapo itakuwa shwari.ni yule yule mkandamizaji idd sniper