Tuesday, August 12, 2008

Baba Mtakatifu ataka kuondolewa kwa majeshi Georgia


Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Baba Mtakatifu wa kumi na sita, ameonya kuwepo ongezeko la wakimbizi na hata watu kuyakosa makazi yao huko Georgia, kutokana na majeshi yaliyo ingia nchini humo kutoka Urusi.


Kutokana na hilo basi, Baba Mtakatifu huyo ameomba kuondolewa kwa majeshi ya kivita nchini humo ili kurudisha amani ambayo inatoweka, na kuwakutanisha viongozi wa Urusi na Georgia, "Ni matumaini yangu makubwa kuwa shughuli hizi za kivita nchini Georgia zitasimamishwa haraka" alisema.


"Ninaialika jumuiya ya kimataifa kwa ujumla na nchi mbalimbali, kusaidia kupatikana kwa suluhisho juu ya tofauti kwa nchi hizi mbili na kuleta amani ya kudumu na kufikia muafaka kati ya pande zote mbili ambao utakuwa wa sawa na haki na wa heshima.




No comments: