Balozi wa Redd's 2008 Angela Lubala, amelirudisha taja lake alilokuwa amelishinda katika kinyang'anyiro cha Vodacom Miss Tanzania 2008.
Angela alisema amefikia uamuzi huo kutokakana na imani yake ya dini ya World Alive International Outreach lililopo Sinza, jijni Dar.
“Nachukua fursa hii kuiambia jamii kuwa kutokana na imani yangu katika Yesu Kristo, sitaweza kuwakilisha Redd’s kama Redd’s Fashion Ambassador 2008, Kwa kuwa mimi si mbinafsi, narudisha taji hili na zawadi zake zote kwa Redd’s, napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Vodacom, Lino na Redd’s kwa uelewa juu ya uamuzi wangu huu”, alisema.
Vodacom ndio wadhamini wakuu wa Miss Tanzania. Angela ambaye pia ni Miss Temeke 2008, alisema zawadi anayorudisha ni fedha sh. Milioni 2.5.
Alipoulizwa kama hakujua wakati anashiriki mashindano hayo tangu mwanzo kama kuna jambo kama hilo, alisisitiza kuwa suala la kuwa Balozi wa kinywaji hicho haliendani na imani yake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comment:
naanza kwa kusema ashakum si matusi wewe sister wakati ulipokuwa unaanza kushiriki,mpaka unapata hilo taji na ww ukalikubali hukujua kama ww mlokole ww huna lolote ulitoa kitu sasa unaona nama ikingundulika unaamua kujiuzulu eee.bora ungewaachia wenzako watoe kitu wapate kitu hata ikigundulika kwao shega sasa ww mambo huyawezi unasingizia dini hiyo sio ishuuuuuuuu ni hayo tu.by sniper
Post a Comment