SISI siyo wanyama, sisi siyo mizimu sisi ni binadamu ni sehemu ya jamii kama wengine ... tukimbilie wapi ili kujiokoa na watu wasio na chembe ya huruma. Ukatili gani tunaofanyiwa au imekuwa makosa sisi kuumbwa hivi?
Hayo yalisemwa kwa masikitiko na mlemavu wa ngozi ambaye pia ni mwanaharakati wa kutetea haki za walemavu, Josephat Toner, wakati akielezea madhara yanayowakumba walemavu wa aina yake.
Toner anasema hali ya maalbino nchini imekuwa mbaya sana kwa kuwa katika maeneo kadhaa wamekuwa wakiwindwa kama wanyama na hivyo kuwafanya waishi kwa hofu kuwaathiri kisaikolojia.
Alitoa mfano wa Mchungaji wa Kanisa la FPCT la Masama, Wilaya ya Hai. mkoani Kilimanjaro, Emmanuel Swai, ambaye amelazimika kuacha kumtumikia Mungu pamoja na familia yake na kwenda mafichoni kufuatia kupokea vitisho kwa njia ya ujumbe wa simu kuwa popote atakapopatikana atauawa na viungo vyake kuchukuliwa.
“Tunaamini serikali ikiamua kulishuhgulikia kikamilifu suala hili, litakoma mara moja lakini mambo yanasuasua," alisema.
No comments:
Post a Comment