WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Prof Jumanne Maghembe alikuwa kivutio kikubwa alipoingia darasani na kufundisha hesabu za desimali katika Chuo cha Ualimu cha Capital cha mjini Dodoma.
Prof Maghembe ambaye alikwenda chuoni hapo Ijumaa wiki iliyopita kukizinduzi rasmi, aliamua kufanya ziara katika majengo hayo na kumkuta mmoja wa walimu wananfunzi akiwafundisha watoto wa darasa la tano somo la hesabu na yeye akaamua kushika chaki na kuanza kufundsisha.
''Watoto mnaonaje tukianza na swali la pili ambalo bado mwalimu wenu hajawafundisha. Haya wewe pale unafikiri tunaanza na kitu gani? Kwanza lazima mtambue kuwa hizi ndizo
hesabu za desimali na mkizifahamu bila shaka hamtapata shida katika mitihani yenu,'' alisema Prof Maghembe wakti akiwafundisha wanafunzi hao.
Baada ya kukagua maeneo ya shule hiyo, Waziri Maghembe alisema ameridhishwa na maelezo aliyopata kutoka kwa mwananfunzi wa mwaka wa pili chuoni hapo kuhusu somo la sayansi.
Mwananfunzi huyo Theresi Lejale alionekana kujiamini na kujibu maswali mengi kutoka kwa Waziri na watu mbalimbali walikuwa wameongozana nao hivyo kumwagiwa sifa kwamba amewafunika hata wanaume kujieleza.
''Huyu binti anaonekana kuwa amekomaa sana na hana wasiwasi na alichokieleza, hivyo sina shaka kabisa huyu akipewa shule anaweza kufundisha, kwa sababu hata ninyi mmeona, kwani licha kuulizwa maswali mengi, karibu yote ameyajibu kwa ufasaha, hongera sana binti,'' alisema Waziri.
-001.jpg)
No comments:
Post a Comment