Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, na afisa mwandamizi mmoja wa upinzani wamesema muafaka wa kugawana madaraka utafikiwa baada ya muda mfupi.
Gazeti linalomilikiwa na serikali ya nchi hiyo, The Herald limeandika kwamba afisa mmoja wa Bw Mugabe alisema nyadhifa zilizopangwa wiki iliyopita huenda zikabadilishwa.
Hata hivyo, kiongozi wa upinzani Morgan Tsvangirai hakuwa na matumaini makubwa akisema mazungumzo hayo yamekuwa ya ubabaishaji.
Aliyekuwa rais wa Afrika Kusini Thabo Mbeki amekuwa akisimamia mazungumzo hayo kwa siku ya pili sasa.
Bw Mugabe na Bw Tsvangirai walitia saini ya mpango wa kugawana madaraka mwezi uliopita.
Lakini viongozi hao wameshindwa kufikia makubaliano ya kugawana nyadhifa katika wizara mbalimbali nchini humo hadi sasa.
No comments:
Post a Comment