Sunday, August 10, 2008

Mnauye aweza ukosa Uenyekiti UVCCM


Nape Mnauye yuko kwenye wakati mgumu katika kinyang'anyiro cha Uchaguzi mkuu wa uenyekiti Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), baada ya hoja ya umri kuibuliwa.

Nape alisema haogopi mchezo mchafu wa wapinzani wake kwa kuwa alipoamua kuchukua fomu alikuwa na akili timamu na akizifahamu kanuni, sheria na katiba ya umoja huo vyema, alisema hayo katika mahojiano na chombo kimoja cha habari.

“Kati ya wagombea wote zaidi ya 20 mimi ndiye mwenye uzoefu mkubwa katika chama na jumuiya ya vijana, nimekuwa mjumbe wa NEC kwa muda wa miaka sita, Mjumbe wa baraza la kuu la UVCCM kwa miaka sita na Katibu Msaidizi Idara ya Siasa Makao Makuu ya Chama, najua kanuni, sheria na katiba ya chama ya umoja wa vijana” alisema.

No comments: