Friday, August 29, 2008

Pinda aongea

SAUTI za minong'ono zilikuwa zimetanda kwenye Ukumbi wa Bunge jana wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alipokamilisha kusoma hotuba yake ya utekelezaji wa mapendekezo ya Kamati ya Richmond, baada ya hatua kadhaa dhidi ya wahusika kumsubiri rais na watendaji wake.

Uwezekano wa wabunge kujiridhisha kwa kuchangia hotuba hiyo mara baada ya Waziri Mkuu kumaliza kutoa hoja, ulishindikana baada ya Naibu Spika, Anna Makinda, kuzima juhudi hizo akisema wataijadili taarifa hiyo katika kikao kijacho cha Novemba, mwaka huu.

Kati ya mapendekezo hayo ni machache tu ndiyo ambayo utekelezaji wake umekamilika huku mengine muhimu ambayo wabunge na wananchi walikuwa wanayasubiri kwa hamu yakiachwa kwa mamlaka zinazowajibika, likiwamo suala la Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kusubiri hatua atakazochukuliwa na Rais Jakaya Kikwete, huku la Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) likiachwa mikononi mwa Katibu Mkuu Kiongozi.

No comments: