Tuesday, August 12, 2008

Shaggy Kipenzi cha wa Tz


LICHA ya kukonga nyoyo za mashabiki msanii Norville Rogers au Shaggy mwisho wa wiki kwenye viwanja vya Leaders, Dar es Salaam alitumia muda huo kukemea vitendo vya ubaguzi wa rangi na kijinsia na kusisitiza upendo.
Msanii huyo aliyezaliwa Jamaica na kuhamia Marekani anakoishi sasa, alikuwa akitumbuiza katika onyesho la uzinduzi wa kampuni mpya ya simu za mikononi ya Zain ambayo awali ilikuwa ikitumia jina la Celtel.
Shaggy ambaye ana albamu kumi hadi sasa, alikonga nyoyo za mashabiki na kila baada ya nyimbo mbili au tatu alikuwa akitoa somo.
"Tusibaguane jamani sisi sote ni binadamu, tusibaguane kutokana na rangi, jinsia au hali yetu ya kimaisha,"alisema msanii huyo ambaye alitumbuiza kwa zaidi ya saa mbili kutokana na shinikizo la mashabiki.

No comments: