Wanafunzi hao, walikumbwa na ugonjwa huo wa ajabu wa kupiga kelele, kuanguka na baadae kupoteza fahamu wakiwa katikati ya mitihani wao wa somo la Sayansi, mara baada ya mwanafunzi mmoja kuanza kwa kupiga kelele na wengine kufuata.
Kutokana na tukio hilo, viongozi na walimu wa shule hiyo walifanya juhudi za kuwapeleka watoto hao Hospitali ya Mkoa ya Kitete na wengine kuwahamishia vituo vingine vya mitihani, lakini pia gazeti hili lilishuhudia wazazi na walezi wakimiminika shuleni hapo huku wengine wakimwaga machozi.
Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Moshi Chang’a, alionekana akijitahidi kuwakamata na kuwapandisha watoto waliokumbwa na tatizo hilo kwenye magari kwa ajili ya kuwapeleka hospitali na wengine katika kituo kipya cha dharura cha Shule ya Sekondari ya Wasichana Tabora.
-001.jpg)
No comments:
Post a Comment