BUNGE la Umoja wa Ulaya (EU), limeeleza kushtushwa na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) yanayoendelea nchini Tanzania na kuitaka serikali ichukue hatua zaidi.
Bunge hilo liliitaka EU kuisaidia Tanzania kuchukua hatua hizo, katika mjadala uliopitishwa kwa kura zote 93. Katika mapendekezo yake bunge hilo, lilikemea vikali mauaji hayo yanayotokana na imani za kishirikina, ambayo hufanywa kwa nia ya kuuza viungo vyao.
Rais Jakaya pamoja na kupewa sifa kwa kumteua mbunge mwanamke albino, Al-Shymaa Kway-Geer kuwa Mbunge wa kwanza albino, nchi za Ulaya zinaitaka serikali yake kuchukua hatua zaidi kuwalinda walemavu hao dhidi ya mauaji ya kinyama.
Uamuzi huo unaitaka serikali na jamii kwa ujumla kushirikiana kwa pamoja kuwalinda maalbino.
Pia unaitaka serikali ya Tanzania kuchukua hatua za haraka za kutoa elimu kwa umma ili kuifanya jamii iwathamini albino kwa kuhakikisha kuwa inatoa elimu hiyo, hasa maeneo ya vijijini ambako watu hawana elimu ya kutosha.
No comments:
Post a Comment