Tuesday, September 2, 2008

Kesi ya Zombe yaanza tena

Kesi ya mauaji ya wafanyabiashara wa madini wa Mahenge inayomkabili Mkuu wa Upelelezi wa zamani wa mkoa wa Dar es Salaam ACP Abdallah Zombe na wenzake jana, imeendelea kuwa kivutio kikubwa huku baadhi ya wafanyakazi karibu na Mahakama Kuu wakifunga ofisi zao ili kufuatilia mwenendo wa kesi hiyo.

Kesi hiyo, ilianza saa 4.30 na Jaji Salum Massati alipoingia katika chumba namba moja, watu waliokuwa wakisubiri kesi hiyo kwa hamu, walikimbilia katika chumba hicho huku wakipigana vikumbo kutafuta nafasi za kukaa.

kuomba kutotajwa majina yao, walisema wametoroka kwa ajili ya kusikiliza kesi hiyo na moja kati yao, alisema anafanya kazi Wizara Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Mkazi wingine wa Kiwalani ambaye pia hakutaka kutaja jina lake, alisema anafanya kazi Kampuni ya ulinzi ya Armor Group (Tz) Ltd) ya jijini Dar es Salaam.

“Sijatoroka kazini, leo niko ‘off’ lakini jioni nitaingia kazini nimekuja kuisikiliza hii kesi kwani nimekuwa nikisoma kwenye magazeti tu, sasa leo nimekuja kabisa ili nijue kinachoendelea,” alisema mfanyakazi wa Armor group.

Naye Athumani Mussa mkazi wa Temeke aliyekuwa nje ya mahakama hiyo, alisema tangu kuanza kwa kesi hiyo, hajawahi kukosa kuisikiliza kwa kuwa ina mvuto na pia kiongozi wa cheo cha juu kufikishwa mahakamani.

Nje ya chumba namba moja ambako kesi hiyo, inasikilizwa kabla ya kesi kuanza, watu wengi walikuwa wamekusanyika ili kusubiri kuanza kwa kesi hiyo huku wengine wakiulizana mwisho wa kesi hiyo, itakuwaje.

Katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, mahakama hiyo ilielezwa na upande wa mashtaka kuwa mshitakiwa wa 11 Koplo Rashidi alishinikizwa na wakuu wake wa kazi, Zombe na Bageni, kutoa maelezo ya uongo kwenye tume ya Polisi na ya Jaji Kipenka.

Shahidi huyo, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Edson Mmari (55) kwa sasa ni Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora na wakati wa tukio hilo alikuwa Mpelelezi wa Makosa ya Kuwania mali, Makao Makuu ya Upelelezi.

ACP Mmari aliieleza mahakama kuwa alikuwa ni mmoja wa maofisa walioteuliwa kuchunguza kesi ya mauaji inayomkabili Zombe na polisi wenzake.

“Baada ya kuteuliwa tuliambiwa washitakiwa wamekamatwa na wako Kituo cha Polisi Kati (Central) hivyo tuliwahoji,”alisema ACP Mmari.


No comments: