Saturday, September 6, 2008

Kikwete kuzuru Sudan na Swaziland

Rais Jakaya Kikwete aliondoka nchini jana mchana kwenda Swaziland na Sudan kwa ziara ya kikazi ya siku nne, imesema taarifa ya Ikulu. Akiwa Swaziland kwa siku tatu, Rais Kikwete aliyeandamana na mkewe, Salma Kikwete atahudhuria sherehe mbili kubwa za kitaifa za miaka 40 zinazojulikana kama “40th National Double Celebrations.” 

Sherehe hizo ni miaka 40 ya kuzaliwa kwa Kiongozi wa nchi hiyo, Mfalme Mswati III na miaka 40 ya uhuru wa nchi hiyo kutoka kwa Waingereza. Sherehe zote mbili zinaangukia na kufanyika leo. 

Rais amepangiwa kuondoka Swaziland kesho kwenda Sudan ambako atafanya ziara nyingine ya kikazi. Akiwa Sudan, Rais Kikwete katika nafasi yake ya Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) atakuwa na mazungumzo na mwenyeji wake, Rais Omar El Bashir. Rais anatarajiwa kurejea nyumbani keshokutwa.

No comments: