RAIS Jakaya Kikwete, ameonya kwamba kama nchi ikiendelea kuzalisha wanasiasa kwa wingi itaishia kwenye malumbano na migogoro isiyo na tija, badala yake amewataka Watanzania kuijenga katika misingi ya sayansi na teknolojia.
Akizungumza kwenye mkutano wa sita wa Siku ya Wahandisi nchini uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, Rais Kikwete alisema njia pekee ya kuiletea nchi maandeleo ni kuzingatia sayansi na teknoliji badala ya siasa ambayo huishia kwenye porojo na malumbano.
Alisema umefika wakati kwa kutumia wataalam hasa wanasayansi kufanisha utendaji badala ya wanasiasa katika mambo yanatakiwa watu waliobobea kwenye fani hizo.
Rais alisema takwimu zinaonyesha kuwa Tanzania ina wahandisi 8,000 ikimanisha kuwa kila mhandisi mmoja anashughulika na Watanzania 5000, jambo ambalo ni hatari kwa maendeleo ya taifa.
"Wasomi wanaeleza kuwa kama mtu anataka kujua maendeleo ya nchi, anaangalia idadi ya wahandisi na ubora wao, kama sisi tuna wahandisi wasiozidi 8,000 na nchi ina watu karibu milioni 39 hapo mambo yanakuwaje?’’alihoji Rais Kikwete.
Alisema nchi ya Japan kila mhandisi mmoja anawahudumia wananchi 54, wakati hapa Tanzania mambo uwiano unaonyesha kwamba mhandisi mmoja huwahudumia watu zaidi ya 8,000.
No comments:
Post a Comment