![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEizgvBi9adRDKviA3WWoNyIwv-PeMWNqMOVtTSNSWq0sFplgVIoN_Q7Ex0eVKm9ENKny2Z3ooiLgvRkG5i_km9XssagFw-HQGISvXtNYTjjsK_Lxcu-SvGhCGccY36V9_7pWtO_etIZWXg/s400/president_benjamin_mkapa.jpg)
Rais Mkapa alisema hayo Jumapili iliyopita baada ya ibada ya misa katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Fransisco Exaveri lililopo Nyakahoja jijini hapa.
Alisema kwa sasa anatumia muda mwingi akisali na kuwataka waumini wa dini mbali mbali nchini kusali zaidi na kuwataka Watanzania kujenga moyo wa upendo miongoni mwao.
Aliongeza kuwa waumini wa kweli mara kwa mara huwaombea wenzao amani na upendo na kwamba amani hiyo huanzia baina ya mtu na mtu, majirani, jamii hadi nchi na nchi.
Alisema kwa sasa anaona ni afadhali aendelee kumwomba Mungu na kueneza jina lake kwa njia ya Biblia, jambo ambalo aliwataka Watanzania kufanya hivyo na kwamba watapata neema zaidi iwapo watafuata mahubiri yake na kuhudhuria ibada za misa mara kwa mara na kuwasamehe
waliowakosea.
"Enzi za mimi kujihusisha na mambo ya siasa zilikoma pale nilipokabidhi madaraka kwa Serikali ya Awamu ya Nne mwaka 2005," alisema Rais Mkapa.
Aidha, alisema hata katika ibada hiyo, hakutarajia kupewa nafasi ya kuwaeleza wananchi jambo lolote na kuongeza kuwa alihudhuria ibada hiyo kama muumini wa kawaida.
Aliwaeleza waumini katika Kanisa hilo huku akitoa mifano ya vifungu katika Biblia, ambavyo vilikuwa vikigusia masuala ya upendo miongoni mwa jamii. Misa hiyo ilihudhuriwa pia na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dkt. Alex
Msekela.
No comments:
Post a Comment