Sunday, September 14, 2008

Mtikila kumpeleka Mkapa Kortini


PAMOJA na kutangaza kujitenga na mijadala ya kisiasa na badala yake kujikita zaidi katika masuala ya kuhamasisha upendo, amani na ucha Mungu, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Bw. Benjamin Mkapa anaendelea kuandamwa na jinamizi linalotokana na kazi za mikono yake alipokuwa Ikulu. 

Akizungumza kwa mara ya kwanza tangu alipofutiwa kesi hiyo, Mtikila amekiri kuwa kipindi alichokuwa ameshitakiwa alikuwa katika wakati mgumu kuendelea na masuala yake ya harakati lakini sasa ataanza na Bw. Mkapa. 

"Ni lazima nimburute mahakamani ili aeleze ni kwa nini alijimilikisha mgodi wa Kiwira na kuuza kwa makaburu Benki ya Taifa ya Biashara (NBC)," alisema Bw. Mtikila na kuongeza kuwa pia kesi hiyo itamtaka Bw. Mkapa aeleze ilikuwaje akabariki Serikali kununua ndege ya Rais kwa dola bilioni 50 wakati thamani halisi ya ndege hiyo ikiwa takribani sh. bilioni sita tu. 

"Kwa haya aliyofanya raia wa kweli hawezi kukubali kuyatenda," alisema Mchungaji Mtikila na kuongeza kuwa ni lazima amfikishe mahakamani haraka sana. 

Akizungumzia kesi aliyokuwa ikimkabili ya kudaiwa kumkashifu Bw. Mkapa alisema kesi hiyo ilifunguliwa katika mazingira ya kisiasa kwa lengo la kumziba mdomo. 

"Serikali ilinifungulia kesi hiyo kwa lengo la kuniziba mdomo nisiseme ukweli, lakini sasa wameufungulia kwa kuniondolea kiwingu nitaanza kuwasha moto," alisema Mchungaji Mtikila 

No comments: