Saturday, September 6, 2008

Pakistan kuchagua Rais Mpya

Pakistan inatarajia kuchagua Rais mpya atakaye iongoza nchi hiyo baada ya Rais wa zamani Pervez Musharraf, kujiuzulu mwezi uliopita.

Asif Ali Zardari, ambaye ni mume wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo aliyeuwawa Benazir Bhutto, ndiye anayetarajiwa kuwa mshindi katika kinyang'anyiro hicho.

Baada ya kifo cha Benazir, Desemba mwaka jana, Zardari aliteuliwa kuwa kiongozi wa chama cha Pakistan People's Party (PPT). 


Asif Zardari akiwa na marehemu mkewe, Benazir Bhutto

No comments: