Saturday, September 6, 2008

Q-Chilla "kupibu" Taarabu

Baada ya kuanzisha bendi yake na hivyo kuwapa mashabiki moyo kuwa sasa msanii Q-Chillah ameamua kuupeleka muziki wa kizazi kipya katika level nyingine yaani(next level),msanii huyo amegeuka tena na kudai kuwa sasa anageukia muziki wa Taarab.

Jambo hilo ambalo limeonekana kuwashangaza wengi kama sio wote,kwa msanii huyo ni kama sinema ya kuigiza kutokana na kauli yake kuwa....amefikia uamuzi huo baada ya kuona muziki wa kizazi kipya unafunikwa na ule wa Taarab kutokana na kuwa na mashabiki wengi zaidi.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya..Aboubakar Katwila maarufu kama Q-Chilla amesema sasa ameamua kufanya muziki wa Taarab kwa kuwa unalipa zaidi ukilinganisha na wa Bongo Flava.

Akijitetea kuhusu hilo...Chillah alisema...unapokuwa kwenye fani ya muziki ni lazima uwe mjanja na kusoma vyema alama za nyakati na ndio maana akaamua kutoka kivingine..na kudai kuwa anaamini kutoka kwake kimwambao kutamtoa kiuhakika.

Katika kudhihirisha nia yake hiyo,hivi karibuni alihudhuria tamasha moja la taarab hapa jijini na kukamua sambamba na wanamuziki wa kundi hlo stejini.



No comments: