Wednesday, September 17, 2008

Twanga Kufanya Mambo Kenya

BENDI ya muziki wa dansi ya African Stars International, maarufu Twanga Pepeta imealikwa kwa ziara ya onyesho maalum jijini Nairobi, Kenya.

Ziara hiyo imetolewa na taasisi ya kimataifa ya African Economic Research Consortium yenye makazi yake Nairobi.

Onyesho hilo ni kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo nchini humo.

Mkurugenzi wa Kampuni ya African Stars Entertainment Tanzania (Aset) inayomiliki bendi hiyo, Asha Baraka alisema kuwa wakiwa Kenya, Twanga watafanya maonyesho mawili kwenye ukumbi wa Intercontinental na katika ukumbi wa hoteli ya Carnivore.

Alisema kuwa mbali na maonyesho hayo mawili yatakayofanywa na bendi yake, pia watatumia fursa hiyo kutambulisha nyimbo mpya zinazotamba hivi sasa katika vituo mbalimbali vya redionchini.

Alizitaja baadhi ya nyimbo mpya zinazotarajia kupigwa na bendi hiyo kuwa ni Sumu ya Mapenzi, Nazi haivunji Jiwe.

ìNinafurahi kuwataarifu kuwa Twanga wamepata mwaliko huu kutokana na ukweli usiopingika kuwa wamejijengea jina nchini humo na hii itakuwa safari yetu ya tatu kwenda Kenya.

Kwa kweli ni mafaniko ambayo tunapaswa kujivunia kuona kwamba muziki wa wazawa unakubalika,îalisema.

Alisema kuwa msafara huo utakuwa na wanamuziki 25 ambao ni pamoja na waimbaji wao mahiri, Abuu Semhando, Hamis Amigolas, Luizer Nyoni na Saleh Kupaza, wakati wanenguaji ni Hamisa Mussa, Omari Mussa na Lilian Tungaraza.

No comments: