Umoja wa Mataifa unatarajia kupeleka msaada wa chakula na dawa kusaidia watu 250,000 waliokimbia mapigano mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Msafara unaopeleka msaada huo unatarajia kutoka mjini Goma na kupelekwa katika eneo linalodhibitiwa na waasi wanaoongozwa na Jenerali Laurent Nkunda.
Mawaziri wa mashauri ya kigeni wa Uingereza na Ufaransa, David Miliband na Bernard Kouchner wametembelea nchi ya Rwanda.
Viongozi hao walifanya mazungumzo na Rais Paul Kagame kama juhudi za kujaribu kumaliza mgogoro huo.
Kabla ya hapo, mawaziri hao walikutana mjini Kinshasa na Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Uingereza na Ufaransa zilitoa wito wa utekelezwaji wa mikataba ya kurejesha amani katika eneo hilo na pia kuwanyang'anya silaha makundi ya wanamgambo.
No comments:
Post a Comment