Tuesday, August 12, 2008

Mgosi ndani ya Taifa Stars

KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, Mbrazil Marcio Maximo, jana alitangaza kikosi cha wachezaji 28 huku akiwarejesha kundini Mussa Hassan Mgosi na kumwita kwa mara ya kwanza kipa Amani Simba.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Maximo alisema uteuzi wake umezingatia kiwango cha mchezaji, umri na nidhamu ya nje na ndani ya uwanja.

Alisema kwa kigezo cha umri, ni katika mkakati wa kuunda kikosi kitakachodumu kwa muda mrefu, hivyo asilimia 60 ya wachezaji ni wa chini ya miaka 23, asilimia 20 wa chini ya miaka 20 huku asilimia 20 wakiwa ni zaidi ya miaka 25.

Nyota waliomo katika kikosi hicho na timu zao katika mabano, ni makipa Ivo Mapunda (Yanga), Amani Simba (Simba) na Farouk Ramadhani (Miembeni).


Mbeki ni Shadrack Nsajigwa, Fred Mbuna, Amir Maftah na Nadir Haroub ‘Cannavaro’ (Yanga), Juma Jabu, Kelvin Yondani na Meshack Abell (Simba) na Salum Sued (Mtibwa).


Viungo ni Henry Joseph Shindika, Jabir Aziz na Adam Kingwande (Simba), Godfrey Boniface na Athumani Idd ‘Chuji’ na Kiggi Makasi (Yanga), Nizar Khalfani (Moro United), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar).


Washambuliaji ni Mgosi (Simba), Uhuru Selemani (Mtibwa Sugar), Jerrison Tegete na Mrisho Ngassa (Yanga). Aidha, Maximo amewaita chipukizi watano kutoka mashindano ya Copa Coca Cola na kikosi cha chini ya miaka 20, ambao ni Jonas Salvatory, Yousuf Soka, Adili Adam, Lambele Jerome na Awasi Issa.

No comments: