Friday, October 17, 2008

Chanjo ya Kupooza Yaleta Matumaini

Ugonjwa wa kupooza unaweza ukatoweka kabisa nchini Nigeria, moja ya maeneo ya mwisho hapa duniani yanayoendelea yanayokumbwa na maradhi hayo.

Watafiti wanasema sababu ya kutoweka ugonjwa huo ni chanjo yake kuboreshwa zaidi.

Watafiti wa chuo cha Imperial cha London kimegundua chanjo iliyozinduliwa hivi karibuni ina uwezo wa zaidi ya mara nne kuwalinda watoto kuliko chanjo za awali.

Wataalamu hao walisema chanjo hiyo inaweza ikatokomeza kabisa 'type 1 polio' inayojulikana zaidi nchini humo iwapo itawafikiwa watoto wengi.

Nigeria ni moja ya nchi nne tu duniani ambayo bado ugonjwa huo haujatokomezwa.

Asilimia 82 ya kesi za maradhi hayo imeripotiwa kuwepo nchini Nigeria.

Ugonjwa huo una athari kubwa sana na huwadhuru watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.

No comments: