Friday, September 19, 2008

Maandamano Dhidi ya Viongozi BAKWATA Ruksa

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limesema kundi la waislamu walioomba kufanya maandamano ya amani kushinikiza kurudishwa madarakani kwa viongozi wa Baraza la Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), wa,eruhusiwa kufanya hivyo, lakini likataka wasimalie maandamano yao kwenye ofisi za baraza hilo.

Kamanda wa Dar es salaam, ACP Suleiman Kova alisema jana kuwa jeshi hilo litatoa ulinzi katika maandamano hayo, lakini akasema waandamanaji hawaturuhusiwa kwenda ofisi za makao makuu ya Bakwata.

"Jeshi la polisi litatoa ulinzi, lakini halitaki kamati hiyo, ifike ofisi ya Bakwata na tunaitaka itafute sehemu nyingine ya kuhitimishia maandamano yao na si kwenye ofisi za Bakwata kwa kuwa kuna vikundi vya siri vilivyoandaliwa ili kuhatarisha amani," alisema Kamanda Kova.

"Hivyo natoa onyo kwa atakayekaidi amri hii, lawama zote zitaelekezwa kwa kamati husika."

Kova alikiri kupokea barua kutoka kwa kamati hiyo, ikiomba ulinzi wa jeshi hilo lakini alisema muda mfupi baadaye alipokea barua kutoka Bakwata inayopinga maandamano hayo kumalizikia kwenye ofisi zao kwa kuhofia uwezekano wa kuvunjika kwa amani.

"Barua tuliyopokea kutoka Bakwata ilitueleza kuwa wamepokea taarifa kuwa kuna vikundi mbalimbali vimeandaliwa na kamati hiyo ili kufanya vurugu," alisema.

"Baada ya kufanya uchunguzi tumebaini pande hizo mbili zinaonekana kupaniana, hivyo hali ya usalama itapotea endapo maandamano hayo, yataishia Bakwata.

"Kingine ni kwamba viongozi wa Bakwata wamekataa kupokea maandamano hayo. Sasa kama wamekataa, kamati hiyo itakwenda kufanya nini wakati haitapokelewa na Bakwata."


No comments: