Saturday, September 20, 2008

Mbeki Awashutumu Wanaotaka Kumng'oa


Rais wa Afrika Kusini Thabo Mbeki ameshutumu kampeni zinazoendeshwa ndani ya chama chake cha cha African National Party (ANC), ambapo kuna wanaochagiza ajiuzulu.

Bwana Mbeki ametoa taarifa akiwashambulia wenye tabia ya kuelekeza matusi dhidi yake.

Amekanusha tuhuma kwamba aliingilia kati kesi ya rushwa iliyokuwa inamkabili kiongozi wa ANC Jacob Zuma.

Taarifa hiyo imetolewa hadharani wakati huu viongozi waandamizi wa ANC wakiwa wanajiandaa kuanza mkutano wao wa siku tatu kujadili mustakabali wa Rais Mbeki.

Bwana Mbeki yupo katika chagizo kubwa la kumtaka ajiuzulu kufuatia uamuzi wa mahakama kwamba kulikuwa na shinikizo la kisiasa katika kesi ya Bwana Zuma.

Kamati Kuu ya Taifa ya ANC, itakayojadili suala hilo na ambayo inaundwa na wajumbe wengi wanaomuunga mkono Jacob Zuma, hata hivyo haina ubavu kumshurutisha Bwana Mbeki kujiuzulu wadhifa wa Urais.

Lakini waandishi wa habari wanasema hata kama hawana uwezo wa kumuondoa katika wadhifa wa Urais, wanaweza kulipeleka suala hilo Bungeni.

No comments: