Friday, September 19, 2008

Obama Apitishwa Rasmi

Seneta Barack Obama, jana alipitishwa rasmi na chama chake cha Democratic kuwa mgombea Urais wa Marekani kupitia chama chake hicho. Endapo atashinda urais, Obama atakuwa ndiye Mzungu Mweusi kuwa rais katika nchi hiyo.

Na mwamba mwenyewe, Bw Obama, aliojitokeza kwa muda mfupi jukwaani baada ya hotuba ya Bw Biden.Hotuba yake ni siku moja baadaye.

Hillary Clinton alikuwa na umuhimu mkubwa katika kuhamasisha wajumbe wamwidhinishe aliyekuwa hasimu wake kuwa mgombea rasmi.

Obama ameweka historia kwa kuwa mgombea wa kwanza mweusi kuteuliwa na chama kikubwa kupigania kiti cha rais wa Marekani.Wengi walishindwa kujizuia machozi.

Kando na pilika pilika za kisiasa, Denver mjini, bidhaa zenye kutangaza mambo ya siasa na wanasiasa wa Democratic zilikuwa zikinunuliwa kwa kasi kubwa.

Bill Clinton alipokelewa kwa wajumbe wote kusimama kwa heshima yake ambapo alihutubia na kuahidi kumwunga mkono kikamilifu Obama, ambaye alimwangusha mkewe katika kura za kupata mgombea wa chama hicho.

Kila la Kheri Obama......

No comments: