"Tunaweza kudumisha demokrasia kwa kukuza na kuimarisha uelewa kwa njia ya mfumo wa utawala unaoruhusu wananchi kushiriki utawala kwa kuchagua wawakilishi wake na kutumia vizuri miundombinu ya demokrasia iliyopo," alisema
"Rushwa na ufisadi ni adui wa demokrasia na maendeleo na demokrasia ya nchini kwetu ina matatizo. Wananchi wanalilia Katiba mpya, CCM na Serikali iliyopo madarakani inabidi iwajibike ili kumaliza tatizo la Katiba yenye misingi mizuri ya demokrasia.
Ili tuwe na demokrasia ya kweli ni lazima tuwe na tume huru, itakayowasiliana na vyama vyote vya siasa, lakini tume ya namna hiyo haipo, kwani mfano mzuri ni Tarime, tangu kutangazwa kwa uchaguzi wa jimbo hilo haijawahi kufanya mkutano hata siku moja na vyama vya upinzani," aliongeza

Bw. Msekwa alisema hayo jijini jana katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Demokrasia, ambapo alitoa salamu za chama chake kwa niaba ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete.
No comments:
Post a Comment