Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amewaambia viongozi wa chama chake kwamba makubaliano ya kugawana madaraka ya siku ya Jumatatu ni fedheha.
Lakini Bwana Mugabe akasema chama chake hakikuwa na njia nyingine baada ya kushindwa uchaguzi wa bunge mwezi Machi.
Bwana Mugabe baadae anatarajiwa kukutana na Waziri Mkuu mteule Morgan Tsvangirai kuzungumzia suala la kugawana nafasi za mawaziri chini ya makubaliano yao.
No comments:
Post a Comment