Monday, September 15, 2008

Ngwea - Kwenda Ulaya si Kitu

Wakati wasanii wa muziki wa Bongo Flava wakiendelea kula matunda ya ziara zao za ulaya wanazofanya kila kukicha,mmoja kati wasanii maarufu ktk fani ya muziki...Albert Mangwea 'Ngwea'.... ameibuka na kukandia vibaya ziara hizo huku akidai kuwa ukijipanga vizuri...unaweza ukaingiza mkwanja wa kutisha hapahapa nyumbani ukilinganisha na wale waendao ulaya.

Akionesha msisitizo kuhusu hilo...Ngwea alisema hata siku moja hatishwi na ziara za wasanii wenzake ambao alisema
hata hivyo wamekuwa wakipata malipo madogo kuliko yale ya hapa nyumbani.

...."We mwenyewe unaona pamoja na kwenda kwao ulaya kila siku...lakini si kila ziara inakuwa na manufaa...wengine
hawarudi na chochote cha maana," alimalizia Ngwair huku akimwacha mwandishi mdomo wazi akiwa haelewi je ni wivu 
au ni kitu ganiiiii.

No comments: