RAIS mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa amesema hana nia ya kuwa askofu wala hauhitaji, isipokuwa yeye ni mcha Mungu wa kawaida kama ilivyokuwa awali.
Mkapa alitoa kauli hiyo juzi katika sherehe za Jubilee ya miaka 100 ya Shirika la Masista la Mtakatifu Benedict lililopo Ndanda Wilaya ya Masasi, mkoani Mtwara. Alitumia nafasi hiyo kueleza kuwa vyombo vya habari vilimnukuu vibaya na kupotosha ukweli juu ya kile alichoongea akiwa katika ibada kanisani mkoani Mwanza wiki moja iliyopita.
“Nilikuwa Chato mkoani Kagera, baada ya hapo nilipitia Mwanza nikiwa njiani kurudi nyumbani….niliporudi nyumbani, mwanangu akaniuliza baba siku hizi unataka kuwa kiongozi wa kidini?...Nikamuuliza kulikoni? ...akanijibu magazeti yameandika hivyo,” alisema Mkapa na kuongeza:
“Kweli siku ya pili nikakuta katuni kwenye gazeti moja inayohusishwa na mimi ikiwa imebeba vitabu vya Biblia….sasa nataka kuwahakikishia kuwa sitaki uaskofu wala siuhitaji, ieleweke hivyo…..mimi ni mcha Mungu wa kawaida kama nilivyokuwa awali,” alisisitiza Mkapa.
“Enzi za mimi kujihusisha na siasa zilikoma pale nilipokabidhi madaraka kwa Serikali ya Awamu ya Nne mwaka 2005,” alinukuliwa Mkapa na vyombo vya habari, akiwaambia waumini wenzake katika Ibada hiyo jijini Mwanza kwenye Kanisa Katoliki la Mtakatifu Francisco Exaveri.

Mkapa katika hotuba yake juzi, aliwasifu masista hao kwa kuinua kiwango cha elimu kwa mikoa ya kusini na Tanzania kwa ujumla, sambamba na jitihada zao za kuboresha huduma za afya, hasa katika kutoa tiba na elimu kuhusiana na ugonjwa wa ukoma uliokuwa umeshamiri katika eneo hilo.
“Mimi binafsi nawashukuruni sana maana ujio wenu una mchango mkubwa kwa kiwango cha elimu niliyoipata ambayo imeniwezesha kuwa kiongozi mwadilifu wa nchi hii... na haya ni matunda yenu,” alisema Mkapa ambaye alisoma Shule ya Sekondari Ndanda iliyokuwa inamilikiwa na kanisa hilo.

No comments:
Post a Comment