Saturday, September 20, 2008

Odemba Kwenda Miss Earth Phillipines

KAMPUNI ya Compass Communication ambao ni waratibu wakuu wa mashindano ya Miss Universe Tanzania wamemteua Miriam Odemba kuiwakilisha Tanzania katika shindano la Miss Earth litakalofanyika nchini Philipines.

Hii itakuwa ni nafasi nyingine kwa Miriam ambaye tayari alishawahi kushiriki katika nyanja ya mitindo kupitia M-Net Face of Africa na kufanya vyema kabla ya kuharibu mkataba wake kulingana vigezo vilivyowekwa.

Akizungumza na Mwananchi, Mkurugenzi wa Compass Communication Inayomwandaa mrembo huyo, Maria Sarungi alisema mrembo huyo atakwenda Philipines mwanzoni mwa mwezi ujao.

"Tunaamini atafanya vizuri kutokana na historia yake ya kushiriki katika nyanja mbalimbali za mitindo na kufanya vizuri hivyo, lazima atakuwa na uwezo wa kuiwakilisha nchi yake popote pale atakapokwenda," alisema 

No comments: