Sunday, September 7, 2008

Stars Yaibuka

KWA mara ya kwanza tangu atue hapa nchini kocha Mbrazil Marcio Maximo ameiongoza Taifa Stars kupata ushindi mnono wa mabao 4-1 katika mchezo wa kukamilisha ratiba dhidi ya Mauritius uliochezwa nchini humo.

Stars ilipoteza matumaini ya kufuzu kwa Fainali za Kombe la Dunia na Mataifa ya Afrika baada ya kumaliza michezo minne ya awali ikiwa ni pointi mbili, timu hiyo ilitoka sare ya bao 1- 1 na Mauritius katika mchezo wa awali uliochezwa hapa jijini Dar es Salaam, ikachapwa na Cape Verde bao 1-0, ikatoka sare ya 0-0 na Cameroon na kukubali kipigo cha mabao 2-1 katika mchezo wa marudiano.

No comments: