Sunday, September 21, 2008

Mbeki Kujiuzulu

Chama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress (ANC) kimemtaka Rais Thabo Mbeki kujiuzulu kutokana na madai ya kula njama dhidi ya kiongozi mkuu wa chama hicho.

Kamati Kuu ya Taifa ya chama hicho, imesema Bwana Mbeki ni lazima ang'atuke baada ya jaji kubainisha aliingilia kesi dhidi ya mpinzani wake, Jacob Zuma.

Kamati hiyo Kuu ya ANC yenye wafuasi wengi wa Bwana Zuma, haiwezi kumlazimisha Bwana MBeki ambaye amekanusha madai hayo, kuondoka madarakani.

Bwana Zuma anapewa nafasi ya kuchukua nafasi ya Bwana Mbeki katika uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika mwakani.

Bwana Zuma alimshinda hasimu wake huyo katika nafasi ya uongozi wa ANC katika uchaguzi uliofanyika mwaka jana, wakati Bwana Mbeki alipomtimua katika nafasi yake ya makamu wa Rais mwaka 2005.

Mapema mwaka huu jaji wa mahakama kuu aliitupilia mbali kesi ya madai ya rushwa iliyokuwa ikimkabili Bwana Zuma, kwa maelezo kulikuwa na ushahidi wa kuingiliwa kisiasa katika uchunguzi wa kesi hiyo.

No comments: