Tuesday, October 28, 2008

Zimbabwe Bado Akieleweki


Maofisa wa serikali ya Zimbabwe wamesema viongozi wa Afrika wanaokutana Zimbabwe wameshindwa kuamua lolote la maana kuumaliza mzozo wa kisiasa wa nchi hiyo.

Mazungumzo ya kugawana madaraka kati ya Robert Mugabe na hasimu wake kiongozi wa upinzani, Morgan Tsvangirai, yamekuwa yakifanyika mjini Harare.

Mchakato wa mazungumzo hayo umekwama kutokana na suala la kugawana wizara muhimu.

Jumuia ya maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika imesema mkutano mkubwa zaidi wa eneo hilo ni muhimu kufanyika kujaribu kumaliza kabisa mzozo wa kisiasa wa Zimbabwe.

Wiki sita zimekwishapita tangu Bwana MUgabe na Bwana Tsvangirai waliposhikana mikono mjini Harare na kutiliana saini kilichoonekana kitendo cha kihistoria cha kugawana madaraka.

Mwandishi wa BBC kusini mwa Afrika Peter Biles amesema jaribio la kuunda serikali ya muungano limeitumbukiza nchi hiyo katika matatizo zaidi.

Siku ya Jumatatu Bwana Mugabe na Bwana Tsvangirai walifanya mazungumzo yaliyodumu kwa saa 13 chini ya muendelezo wa mpatanishi wa mazungumzo hayo, aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini na pamoja na viongozi wa Afrika Kusini, Angola, Msumbiji na Swaziland.

No comments: